Thursday, July 25, 2013

Treni ya Mwakyembe yarejea tena kazini


Usafiri wa gari moshi katikati ya jiji la Dar es salaam maarufu kama Treni ya Mwakyembe umerejea na unaendelea kufanya safari zake kama kawaida baada ya kuharibika na kushindwa kufanya kazi wa siku kadhaa. Wakiongea na ITV baadhi ya wakazi wa jiji la Dar es salaam wanaotumia usafiri huo wameshauri kuwa ni vyema usafiri huo ukaimarishwa kimiundombinu ili kuwapunguzia wakazi adha kwa kuharibika mara kwa mara.

0 comments:

Post a Comment