Mke wa mjukuu wa mfalme wa Uingereza, Prince William
amejifungua mtoto wa kiume katika hospitali ya St.Mary's, Paddington
Mashariki mwa mji wa London.
Katika taarifa ya Kasri la kifalme la
Kensington, Duchess wa Cambridge amepata mtoto wake wa kwanza majira ya
saa kumi na dakika ishirini na nne za jioni kwa saa Uingereza,akiwa
amezaliwa na kilo 3.62874.
Kasri la Kifalme limesema, mama na mwanawe wanaendelea vyema na watasalia hospitalini usiku huu.
Baba wa Mtoto, Prince William alishuhudia wakati mtoto akizaliwa.
Tangazo la kuzaliwa kwa mtoto limetolewa na
kuonyeshwa mbele ya lango kuu la Kasri kuu la kifalme la Uingereza la
Buckingham kama utamaduni na mila za Uingereza zilivyo.
Taarifa rasmi iliyosainiwa na jopo la madaktari
bingwa kuthibitisha kujifungua kwa Duchess wa Cambridge ilipelekwa
kwenye kasri la kifalme chini ya ulinzi wa polisi.
Malkia wa Uingereza,Duke wa Edinburgh,Prince wa
Wales, Duchess wa Cornwall na Prince Harry pamoja na wanandugu wa
familia zote wametaarifiwa juu ya kujifungua salama kwa Kate na wote
wamepokea vizuri habari hii, Imesema taarifa hiyo ya Kasri la kifalme.
Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameron
ameandika kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter ujumbe wa kuwapongeza
Prince William na mkewe kwa kupata mtoto wa kiume na kusema nchi nzima
itashangilia kwa ujio wa mtoto wa kiume.
Kiongozi wa chama cha Labour Ed Miliband pia
ameandika kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter "pongezi nyingi kwa Duke
na Duchess wa Cambridge. Nawatakia wao na mtoto wao furaha na afya
njema."
Source :BBC Swahili
0 comments:
Post a Comment