Alisema
hayo alipozungumza kwenye mkutano wa hadhara mjini Songea juzi, katika
ziara yake ya wiki moja mkoani Ruvuma, baada ya kuutembelea mkoa mpya wa
Njombe.
“Ni
kama vile tozo iliyoongezwa kwenye mafuta ya petroli, ambayo imetupa
fedha nyingi kwenye Mfuko wa Barabara, za kuunganisha miji na mikoa na
nyingi zimejengwa na zinaendelea kujengwa.
“Nani
asiyetaka vijiji vipate umeme kama miji, ili usaidie kuondoa giza,
uendeshe viwanda vidogo vidogo na usaidie kukuza uchumi?Wanaopinga tozo
hii, hawatutakii mema,” alisema Pinda.
Bunge
la bajeti lililomalizika mwezi uliopita, lilipitisha tozo ya Sh 1,000
kwa matumizi ya simu za mikononi, ili fedha zitakazopatikana zisaidie
katika mpango mkubwa wa kueneza umeme vijijini unaoendeshwa na Wakala wa
Umeme Vijijini, (REA). Kwa mkoa wa Ruvuma peke yake, vijiji vipatavyo
150 vitapatiwa umeme chini ya mpango huo.
Katika
mikoa yote nchini kuna idadi inayotofautiana ya vijiji vingi
vitakavyonufaika katika mpango huo. Umeme umo katika sekta ya nishati
ambayo ni moja ya sekta sita zilizoteuliwa kutekelezwa chini ya mpango
wa kuhakikisha matokeo makubwa yanapatikana sasa, wenye upeo wa miaka
mitatu, kuanzia mwaka huu wa fedha wa 2013/14. Sekta nyingine ni Kilimo,
Uchukuzi, Maji, Elimu na Mapato.
Kabla
ya mkutano wa hadhara, Waziri Mkuu alizindua Chuo cha Mafunzo ya Ufundi
Stadi cha Songea, kinachodahili zaidi ya wanafunzi 500 na kutoa mafunzo
ya muda mfupi kwa mfundi stadi mbalimbali.
Awali
Waziri Mkuu Pinda alisema bei ya mahindi kutoka kwa mkulima katika mkoa
wa Ruvuma, itakuwa ni Sh 500 kwa kilo badala ya Sh 450, ili wakulima
wahamasike kuuza mahindi kwa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula
(NFRA).
Mkoa
wa Ruvuma ni moja ya mikoa inayozalisha mahindi, chakula kikuu nchini
kwa wingi na NFRA inatarajia kununua tani 50,000 kutoka katika mkoa huo.
NRFA
imepangiwa kununua zaidi ya tani 200,000 nchini kote kwa ajili ya
hifadhi ya chakula, kiwango kikubwa kuliko mwaka uliopita.
Katika
hatua nyingine, Waziri Mkuu Pinda pia aliweka jiwe la msingi la ujenzi
wa soko la kimataifa katika kijiji cha Mkenda kwenye mpaka na Msumbiji,
ikiwa ni moja ya masoko 48 yatakayojengwa mipakani kurahisisha biashara
na kukabiliana na magendo. Leo Waziri Mkuu ataondoka Songea kurejea Dar
es Salaam baada ya kumaliza ziara yake mkoani humo.
0 comments:
Post a Comment