Monday, June 30, 2014

Madereva wa mabasi makubwa ya abiria wagoma


Baadhi ya Madereva wa mabasi makubwa yanayosafirisha abiria kutoka mikoa mbalimbali kupitia mkoani Singida, hapo jana waligoma kuendelea na safari zao kufuatia madai yao ya kunyanyaswa na baadhi ya askari wa usalama barabarani mkoani SINGIDA.

Maderva hao wamesema tuhuma za kuombwa rushwa imekuwa ni miongoni mwa manyanyaso wanayoyapata kutoka kwa askari wa usalama barabarani mkoani Singida.

Kamanda wa kikosi cha usalama barabarani mkoani wa SINGIDA ,MOHAMED LIKWATA alifanikiwa kuwashawishi madereva hao kuendela na safari baada ya kuzungumza nao kwa zaidi ya dakika 45.

0 comments:

Post a Comment