Monday, June 30, 2014

Viongozi vyama vya msingi vya ushirika kuchukuliwa hatua za kisheria


Wizara ya Kilimo, Chakula na ushirika imesema itawachukulia hatua za kisheria baadhi ya viongozi wa vyama vya msingi vya ushirika vya zao la pamba katika Halmashauri ya USHETU, wilayani KAHAMA mkoani SHINYANGA watakaobainika kujihusiha na ubadhirifu wa fedha za malipo ya wakulima wa tumbaku kupitia vyama vyao.

Akizungumza na baadhi ya wakulima katika kijiji cha USHETU katika Halmashauri hiyo, Naibu Waziri wa Kilimo , Chakula na ushirika GODFREY ZAMBI amesema hatua hiyo imetokana na kilio cha muda mrefu cha wakulima wa tumbaku kushindwa kulipwa fedha za mauzo ya tumbaku zao kwa wakati.

0 comments:

Post a Comment