Sunday, June 29, 2014

NKWABI NG’WANAKILALA afariki dunia


Aliyekuwa mkurugenzi mkuu wa Radio Tanzania Dar es salaam (RTD) NKWABI NG’WANAKILALA amefariki dunia katika hospitali ya rufaa ya bugando jijini mwanza alikokuwa amelazwa kwa matibabu.

Mtoto wa marehemu NG’WANAKILALA, LUGENDO NG’WANAKILALA amethibitisha kutokea kwa kifo cha baba yake ambapo amesema mwili wa marehemu unatarajiwa kusafirishwa siku ya jumatatu kwenda jijini dar es salaam kwa ajili ya mazishi.

Marehemu NG’WANAKILALA kabla ya kupatwa na mauti hayo alikuwa mhadhiri katika chuo kikuu cha mtakatifu augustino (SAUT) jijini mwanza.

Source: TBC1

0 comments:

Post a Comment