Sunday, June 29, 2014

Serikali yajipanga kuimarisha mtengamano wa kiuchumi


Waziri mkuu MIZENGO PINDA amesema serikali imejipanga kuimarisha mtengamano wa kiuchumi na mwenendo wa ukuaji wa uchumi wa Taifa ili kuboresha maisha kwa wananchi.

Waziri mkuu PINDA ameyasema hayo bungeni mjini DODOMA wakati akiahirisha mkutano wa bunge la bajeti ambapo amesema hatua hiyo itawasaidia wananchi wa kipato cha chini katika maeneo ya vijijini katika kuinua uchumi wao.

Bunge lilipitisha muswada wa sheria ya fedha wa mwaka 2014 ambapo awali waziri wa fedha SAADA SALUM MKUYA akijibu hoja za muswaha huo pamoja na mambo mengine amezungumzia mpango wa serikali kuwapunguzia kodi wafanyakazi na nyongeza ya mishahara

0 comments:

Post a Comment