Jeshi la Misri limeonya kuwa litatumia nguvu dhidi ya makundi yatakayosababisha ghasia na machafuko wakati wa maandamano ya leo.
Mkuu wa majeshi Jenerali Abdel
Fattah al-Sisi ametoa wito kwa raia wa nchi hiyo kuandamana katika b
arabara za mji kuunga mkono juhudi zao za kukabiliana na vitendo vya
kigaidi.
Wafuasi wa rais aliyeondolewa madarakani, Mohamed Morsi vile vile wanatarajiwa kushiriki katika maandamano hayo.
Bwana Morsi amekuwa akizuiliwa na jeshi tangu tarehe tatu mwezi huu.
Mwendesha mashtaka mkuu wa serikali
amesema, Bwana Morsi anazuiliwa kuhusiana na uhusiano na wapiganaji wa
Kiislamu wa Hamas nchini Palestina.
Shirika la habari la serikali, Mena,
limesema Bwana Morsi anachunguzwa kufuatia madai kuwa anashirikiana na
kundi hilo la Hamas kushambulia vituo kadhaa vya polisi na magereza
wakati wa mageuzi ya mwaka wa 2011.
Lakini chama chake cha Muslim
Brotherhood, kimesema kuwa kilipata msaada kutoka kwa raia wa nchi hiyo
kushambulia magereza na wala sio raia wa kigeni kama inavyodaiwa.
Kiongozi huyo kwa kwanza kuwahi
kuchaguliwa kwa njia ya Kidemokrasia kuongoza Misri, aliondolewa
madarakani baada ya raia wa nchi hiyo kuandamana wakati wa sherehe za
kuadhimisha mwaka mmoja tangu alipochukua madaraka.
Tangu wakati huo, Bwana Morsi amekuwa akizuiliwa na jeshi la nchi hiyo katika eneo lisilojulikana.
Shirika hilo la Mena limesema agizo lilitolewa kwa rais huyo kuzuiliwa kwa muda wa siku kumi na tano.
Msemaji wa jeshi Kanali Ahmed
Mohammed Ali amesema jeshi la nchi hiyo litaruhusu maandamano ya amani
lakini ameonya kuwa watakabiliana vikali na kundi lolote ambalo
litajaribu kusababisha machafuko.
Source : BBC Swahili
0 comments:
Post a Comment