Showing posts with label Kimataifa. Show all posts
Showing posts with label Kimataifa. Show all posts

Wednesday, July 2, 2014

Watu 18 wauawa katika mlipuko Nigeria.




Takriban watu 18 wameripotiwa kuuawa katika mlipuko uliotokea sokoni mjini Maiduguri Kaskazini mwa Nigeria.
Watu walioshuhudia tukio hilo wamesema kuwa gari lililokuwa limebeba mkaa lilipuliwa na bomu linalodhaniwa liliwekwa ndani ya gari hilo.
Hadi sasa hakuna kundi lolote la kigaidi lililokiri kufanya shambulio hilo.

Tukio hili linakuja huku ripoti ya hivi karibuni ya jeshi la Nigeria ikisema kuwa limeshambulia moja ya ngome za kundi la wapiganaji la Boko Haram.

Tuesday, July 1, 2014

Uingereza yakumbwa na uhaba wa mbegu za kiume


 Uingereza inakabiliwa na upungufu wa Mbegu za kiume hali ambayo huenda ikalazimu kiliniki za matibabu ya uzazi nchini humo kuchukua mbegu duni.
Onyo hili limetolewa na shirika la kijamii la matibabu ya uzazi nchini humo BFS.
 
Inadaiwa kuwa baadhi ya kliniki hizo hutegemea shahawa kutoka nchi za kigeni kutokana na mahitaji yake nchini humo.
Lakini mwenyekiti wa shirika hilo Daktari Allan Pacey amesema kuwa ana wasiwasi kwamba baadhi ya vituo hivyo vya matibabu sasa vinatumia kila njia ili kupata wafadhili wa mbegu hizo.
 
Amesema kuwa wanawake watakabiliwa na mbinu zitakazogharimu kiasi kikubwa cha fedha iwapo mbegu duni zitatumiwa.
 
Inadaiwa kuwa upungufu huo unasababishwa na kuondelewa kwa sheria kwamba majina ya wanaotoa mbegu hizo sasa ni sharti yajulikane ikilinganishwa hapo awali ambapo watu wengi walipendelea kuficha majina yao.
Mahitaji ya wafadhili wa shahawa yanazidi kushuka kwa kuwa maendeleo ya matibabu ya uzazi yanawafanya wanaume wengi kutafuta watoto wao wenyewe.
 
Hata hivyo uhaba wa wafadhili wa mbegu za kiume bado upo.
 
Takwimu kutoka mamlaka ya kudhibti uzazi wa binaadamu zinaonyesha kuwa moja kati ya mbegu nne za kiume zimetoka katika mataifa ya kigeni.
Takwimu hizo zilikuwa moja katika kila mbegu kumi mnamo mwaka 2005.

Monday, June 30, 2014

Maiti 30 zapatikana ufuoni Italia


Jeshi la wanamaji nchini Italia , limepata maiti 30 katika mashua ya uvuvi ambayo ilikuwa imewabeba mamia ya wahamiaji haramu.

Mashua hiyo ilipatikana katika eneo moja lililo kati ya mji wa Siciliy nchini Italia na Kaskazini mwa pwani ya Afrika.

Wahamiaji waliofariki walisemekana kufariki kutokana na kukosa hewa.

Ugunduzi huo ulifanyika wakati waokoaji walipotumia mashua hiyo kutaka kuokoa idadi kubwa ya watu waliosemekana kuwa katika hali ngumu baharini.

Miongoni mwa watu hao walikuwa wanawake wawili wajawazito.

Wanajeshi hao walisema kuwa mwishoni mwa wiki waliwaokoa zaidi ya watu hamsini waliokuwa wanajaribu kuvuka na kuingia Italia kutoka Kaskazini mwa Afrika.


Idadi hiyo ya wahamiaji ilitolewa baada ya habari kutolewa kuhusu maiti zilizopatikana.

Wanajeshi hao walisema kuwa watu waliofariki, walifariki kuokana na kukosa hewa kwani walikuwa katika sehemu ya chini ya mashua hiyo.

Mashua hiyo ilikuwa imewabeba takriban wahamiaji 600.

Mkasa wa huo unaonyesha hatari inayowakumba watu wanaotumia kila njia kufika barani ulaya ikiwemo kutumia vyombo ambavyo ni tishio kwa maisha yao.

Italia kwa mara nyengine imesema kuwa mataifa mengine ya ulaya hayafanyi lolote ili kulisaidia taifa hilo kuzuia maafa kama hayo.

Friday, August 9, 2013

"ZIWA NYASA LOTE NI MALAWI, TANZANIA HAINA HATA PUNJE YA ENEO".... MGOMBEA URAIS NCHINI MALAWI AFUNGUKA


Mgombea Urais wa Democratic Progressive Party (DPP) nchini Malawi, Peter Mutharika, amesema hakuna sababu za kufanya majadiliano kuhusu Ziwa Malawi ambalo Tanzania wanaliita Ziwa Nyasa.

Mutharika, ambaye ni mwanasheria, aliyasema hayo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika juzi Mkoa wa Kati.

Akikaririwa na gazeti la Nyasa Times, Mutharika alisema Tanzania haina cha kuambulia kwa Ziwa Malawi.

Kiongozi huyo ambaye hakuwapo katika mkutano wa Rais Joyce Banda na wapinzani kuzungumzia mustakabali wa ziwa, aliwahakikishia Wamalawi kuwa wasiwe na wasiwasi wa mvutano huo.

Mutharika ziwa lote ni mali ya Malawi na akisisitiza kuwa, Tanzania haina hata punje ya eneo.

“Hakuhitajiki majadiliano, Ziwa Malawi ni mali ya Malawi, litakuwa la Malawi,” alisema Mutharika ambaye alichukua masomo ya Sheria Tanzania.

“Tanzania inatumia nafasi ya udhaifu wa uongozi wetu, lakini ukweli, hawana hata tone la eneo... Tutakapoitwa kwenye uchaguzi ujao mwakani, tutamaliza haya yote.

"Nitaleta meli nyingi kwa ajili ya maendeleo ya uchumi, kutengeneza ajira za kutosha kwa vijana,” alisema Mutharika huku akishangiliwa na wafuasi wake.

Tanzania inataka kugawana ziwa, lakini Malawi imegomea mpango huo na suala hilo liko katika majadiliano ambayo Banda alisema kama mwafaka haukupatikana ifikapo Septemba 30, Malawi itapeleka suala hilo Mahakama ya Kimataifa (ICJ).

Sunday, August 4, 2013

WABUNGE WACHAPANA NGUMI ZA KAVU KAVU BUNGENI


Picha: Ni wabunge wa Taiwan 'walivyoadabishana' jana baada ya kupishana maelewano kufuatia mpango wa kupiga kura ya maoni iliyoazimia kuidhinisha umaliziwaji wa mradi wa nne wa Nyuklia katika kisiwa ambacho kinakaliwa na watu wapatao milioni 23.



Saturday, August 3, 2013

Breaking News: Hatimaye Mugabe aibuka kidedea


Rais Robert Mugabe ameshinda kwa mara ya saba, maafisa wanasema, huku kukiwa na madai ya udanganyifu katika uchaguzi.

Bw Mugabe,  ameshinda asilimia 61% ya kura, dhidi ya Waziri Mkuu Morgan Tsvangirai mwenye asilimia 34%.

Bw Tsvangirai amesema uchaguzi haukua wa haki na kulikua na udanganyifu mwingi.Na pia anesema MDC hawata shilikiana na Zanu-PF ,pia wanajiandaa kwenda mahakamani..

Huku matokeo ya mwisho ya uchaguzi mkuu yakisubiriwa, tume ya uchaguzi ya Zimbabwe inasema chama cha Rais Robert Mugabe, ZANU-PF, kimepata thuluthi mbili za viti.



Inamaanisha ZANU-PF ina viti vya kutosha kuweza kubadilisha katiba.
Mpinzani mkuu wa ZANU-PF, chama cha MDC, kimekuwa na kikao kuamua mikakati ya siku za usoni.
MDC inasema haitakubali matokeo ya uchaguzi kwa sababu ya udanganyifu mkubwa katika upigaji kura.
Inaarifiwa kuwa afisa mmoja wa tume ya uchaguzi amejiuzulu, na ametaja ulalamishi katika kura.
Makundi mawili ya Afrika ya wasimamizi wa uchaguzi, kwa jumla yameunga mkono uchaguzi ingawa yameeleza wasi-wasi kuhusu idadi ya wapigaji kura bandia, na kwamba baadhi ya wapigaji kura hawakuruhusiwa kupiga kura.
Source: BBC

Robert Mugabe aongoza kwa kishindo


"Matokeo ya mwisho ya uchaguzi mkuu yakisubiriwa, tume ya uchaguzi ya Zimbabwe inasema chama cha Rais Robert Mugabe, ZANU-PF, kimepata thuluthi mbili za viti."

Inamaanisha ZANU-PF ina viti vya kutosha kuweza kubadilisha katiba.

Mpinzani mkuu wa ZANU-PF, chama cha MDC, kimekuwa na kikao kuamua mikakati ya siku za usoni.
MDC inasema haitakubali matokeo ya uchaguzi kwa sababu ya udanganyifu mkubwa katika upigaji kura.
Inaarifiwa kuwa afisa mmoja wa tume ya uchaguzi amejiuzulu, na ametaja ulalamishi katika kura.

Makundi mawili ya Afrika ya wasimamizi wa uchaguzi, kwa jumla yameunga mkono uchaguzi ingawa yameeleza wasi-wasi kuhusu idadi ya wapigaji kura bandia, na kwamba baadhi ya wapigaji kura hawakuruhusiwa kupiga kura.

Friday, August 2, 2013

Uruguay: Bangi ruksa....


Bunge la Uruguay limepitisha mswada wa kuhalalisha bangi. Ikiwa mswada huu utapitishwa na Baraza la Senate, Uruguay itakuwa nchi ya kwanza kuhalalisha uzalishaji na utumiaji wa bangi.

Hatua hii inaungwa mkono na serikali ikisema itapunguza mapato na faida kubwa kwa walanguzi wa mihadarati pamoja na kuwafanya watumizi wa bangi kutotumia dawa kali za kulevya.Chini ya mswada huo ni serikali pekee itakua na kibali cha kuuza bangi.

Pia serikali itatoa utaratibu wa uzalishaji, mavuno, uhifadhi na mauazo ya nje. Wanunuzi wote watanakiliwa kwenye daftari maalum na sharti wawe wametimiza miaka 18 na zaidi. Mteja anaweza tu kununua kilo 40 kwa mwezi kutoka kwa maduka ya dawa au kukuza mimea sita ya bangi.Wageni hawatakubaliwa kununua bidhaa hii.

Wabunge 50 kati ya 96 walipitisha mswada huo. Wanaotetea kuhalalishwa kwa bangi wamesema vita dhidi ya mihadarati havijapiga hatua na ipo haja kuweka mbinu mpya.

Kwa miongo mingi kanda ya Latin America imekumbwa na ghasia za magenge ya mihadarati ambapo maelfu ya watu wamekufa. Matukio ya Uruguay yanatazamwa kwa karibu eneo hilo ikiwa yatasaidia kupunguza machafuko yanayotishia uthabiti wa mataifa mengi.


Thursday, August 1, 2013

Chama cha Rais Mugabe chajitangazia Ushindi


Chama cha Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe, ZANU -PF leo kimesema kimeibuka na ushindi wa kishindo kwenye uchaguzi uliofanyika jana. Ushindi huo utamfanya Mugabe aiongeze nchi hiyo kwa miaka mitano mingine.

Hata hivyo mpinzani wake wa karibu amesema kura zimeibiwa.Matokeo rasmi ya uchaguzi huo yanatarajia kutangazwa August 5. Chanzo kilicho karibu na Mugabe mwenye umri wa miaka 89, kimeiambia Reuters kuwa majibu yako wazi.

“Tumeshinda uchaguzi. Tumeizika MDC. Hatukuwa na mashaka yoyote kuhusu kushinda,” kilisema chanzo hicho.

Akijibu madai hayo, waziri mkuu nchi hiyo Morgan Tsvangirai ambaye ni mpinzani mkuu wa Mugabe kwenye uchaguzi huo, ameuelezea kama wa ulaghai. MDC kilipanga kuwa na mkutano wa dharura leo.

Masaa 48 waliopewa waasi wa M23 wafika ukingoni


Muda wa saa 48 wa kusalimisha silaha kwa waasi wa March 23(M23), Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo umemalizika na wakati wowote mapigano yanaweza kuanza.

Misheni ya Kutuliza Amani ya Umoja wa Mataifa(Monusco) , ilitoa saa hizo zinazomalizika leo na Jeshi la UN litaanza kutumia nguvu kunyang’anya silaha waasi hao.

Taarifa ya Monusco iliyotolewa na Msimamizi wa Misheni hiyo, Luteni Jenerali Carlos Alberto dos Santos Cruz na kusambazwa na Idara ya Mawasiliano ya Umoja wa Mataifa jana, inaeleza kwamba, watu binafsi katika eneo la Kivu ya Magharibi ambalo linajumisha Goma na Sake na ambao hawahusiki na vyombo vya usalama wamepewa saa 48 kuanzia saa kumi jana (juzi) kwa saa za Goma (Jumanne) kuzisalimisha silaha zao.

Taarifa ilisema, “Baada ya saa 10 jioni ya Alhamisi, Agosti Mosi, wale wote ambao watakuwa hawajasalimisha silaha zao watachukuliwa kama tishio kwa usalama wa wananchi na Monusco itachukua hatua zote muhimu kuwapokonya silaha hizo ikiwa ni pamoja na kutumia nguvu kama ilivyoainishwa katika mamlaka na sheria za ushiriki za Monusco.”

Kwa mujibu wa taarifa hiyo zaidi ya wananchi milioni moja wanaishi katika eneo dogo la Goma na Sake na kandokando ya barabara ambayo inawaunganisha na kambi ya wakimbizi ya Mugungu ambayo ni makazi ya muda ya watu karibu 70,000 ambao wameyakimbia makazi yao kutokana na mapigano.

Kwa mujibu wa Monusco,tangu katikati ya Mei eneo hilo limeshuhudia mapigano ya mara kwa mara kutoka kwa Kundi la M23 dhidi ya Majeshi ya Serikali ya FARDC ikiwa ni jaribio la wazi la kutaka kusonga mbele kuelekea Goma na Sake.

“Katika mashambulizi hayo,likiwamo la hivi karibuni la Julai 14, M23 walitumia kiholela silaha zao za moto zikiwamo silaha nzito ambazo zimesababisha wananchi kujeruhiwa.”

Taarifa hiyo imeongeza kwamba kundi hilo la M23 katika mashambulizi hayo limelenga pia Vituo vya Umoja wa Mataifa.

Taarifa hiyo inabainisha kwamba eneo hilo maalumu la usalama (security zone)litasaidia kudhibiti tishio la moja kwa moja mbali na eneo la nje ya Goma na pengine eneo hilo linaweza kupanuliwa na kurudiwa sehemu nyingine kutakako hitajika.

Tamko hilo la kutoa saa 48 kwa waasi kusalimisha silaha zao linafuatia kuwasili katika eneo la Goma kwa Kamanda Mkuu wa Monusco, Luteni Jenerali Carlos Alberto dos Santos Cruz ambaye alitangaza kwamba Misheni ya Monusco itaunga mkono Jeshi la Serikali(FARDC) katika kuanzisha eneo la usalama kuzunguma eneo la Goma na vitongoji vyake.