Showing posts with label Movies. Show all posts
Showing posts with label Movies. Show all posts

Saturday, July 12, 2014

Mke wa mtu ni SUMU....


STAA wa kitambo kwenye tasnia ya filamu za Kibongo, Stanley Msungu amenaswa laivu akiwa kwenye pozi tata na mke wa mtu aliyetambulika kwa jina moja la Bonita.

Tukio hilo lilijiri nje ya Mgahawa wa Great Wall uliopo Masaki jijini Dar, usiku wa saa saba ambapo kulikuwa na tafrija ya chakula cha usiku iliyoandaliwa na Mwenyekiti wa Bongo Movie Unity, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’.

“Dah! Kuna watu wana uhuru kweli na ndoa zao, yaani Bonita amefunga ndoa juzijuzi tu, mumewe amelala nyumbani yeye anahangaika huku na Msungu.

“Kama huamini nenda kwenye gari ukajionee wanachofanya Msungu na Bonita au hadi tufanye sisi ndiyo mnatupiga picha?” alihoji mmoja wa waigizaji walioalikwa kwenye hafla hiyo ambaye jina tunalihifadhi akimsisitiza mwanahabari wetu kwenda kunasa tukio hilo.

Baada ya kunyetishiwa ishu hiyo, Risasi Jumamosi kama kawaida yake lilinyata hadi lilipokuwa gari la Msungu kisha kunasa tukio hilo ambapo Bonita alikuwa akijificha asionekane vizuri huku Msungu akiwa katika hali ya kutaharuki.

“Kaka mke wa mtu huyu, utaniharibia mimi na yeye kwa mumewe, achana na hayo mambo kaka njoo tuzungumze,” alisema Msungu



Thursday, July 3, 2014

Flora hofu tupu....


Hivi karibuni mumewe, Hamis Baba ‘H. Baba’ kuugua ugonjwa wa homa ya Dengue ‘Dengi’ na kulazwa Muhimbili, msanii wa filamu Bongo, Flora Mvungi amesema alijikuta kwenye wakati mgumu kuhofia mumewe angepoteza maisha.


Flora alisema ni Mungu tu mumewe kupona kwani alikuwa katika hali mbaya ambayo mpaka yeye kama mkewe alikuwa na hofu kubwa ya kifo haswa ukizingatia vifo vya wasanii vilivyotokea mfululizo.

“Nilipoona wasanii wenzangu wakifariki dunia na mume wangu kuzidiwa mpaka kulazwa Muhimbili, nilikuwa nina hofu kubwa ya kifo lakini namshukuru Mungu amepona na tunaendelea na maisha kama kawaida, dengue noma sana,” alisema Flora.

Saturday, August 3, 2013

Filamu ya Irene Uwoya "QUESTION MARK" yatoka rasmi


Katika tasnia ya filamu nchini, jina la Irene Uwoya sii geni hata kidogo lakini filamu hii ya "Question Mark" ni ndiyo inayokufanya utahamaki zaidi kumtazama mwanadada Irene Uwoya.

Kwa habari zilizoifikia site hii ni kuachiwa kwa filamu mpyaaa ya muigizaji maarufu nchini anayekwenda kwa jina la Irene Uwoya, Filamu inaitwa"Question Mark" inapatikana sokoni.

Friday, August 2, 2013

Chanzo chabainika kati ya Shilole na Barnaba


Baada ya siku nyingi kupita tangu Shilole na Barnaba watemane,imebainika kuwepo kwa siri kubwa zilisababisha wawili hao watemane ....

Chanzo cha karibu na Barnaba kimedai kuwa sababu zilizosababisha wawili hao kutemana ni pale shilole alipodanganya umri wake na kumwachia Barnaba jukumu la kumlelea watoto wake...

"Suala la kulea watoto wasio wa kwake lilikuwa ni gumu sana kwa Barnaba kwani wakati huo ndo kwanza alikuwa anaanza maisha na hakuwa na uwezo wa kumhudumia mtu na wanae"..Kilisema chanzo hicho.

Chanzo hicho kiliendelea kufunguka kuwa Shilole ndiye aliye mtongoza Barnaba kwa staili ya kumdanganya umri huku akimweleza kuwa swala la watoto wake lilikuwa linasimamiwa na baba yao.

Habari zinadai kwamba, baada ya Barnaba kuingizwa mkenge, penzi lao lilikuwa kwa kasi sana huku Shilole akijitahidi kuuficha ukweli kwa muda mrefu.

"Cha ajabu ni kwamba, kadri siku zilivyozidi kusonga mbele, Shilole alijisahau na kuanza kumwachia mzigo wa kuilea familia yote..

"Aidha, Shilole aliusahau uongo wake na akajichanganya kutoa historia ya maisha yake katika gazeti moja la udaku ambako alitaja umri wake halisi huku akisimulia jinsi alivyobakwa hadi kupata mimba .Jambo hilo lilimstua sana Barnaba"..Kilisema chanzo hicho na kuongeza:

"Kipengele cha kubakwa kilimchanganya sana Barnaba akawa anajiuliza, kama alibakwa na kupata mtoto,matunzo ya mtoto anayapataje kwa mtu aliyembaka

"Tukio hilo lilo lilimfanya Barnaba apoteze imani na ndipo alipoanza alipoanza kutafuta visa vya kumtema Shilole"

Shilole alipotafutwa kuzungumzia suala hilo hakuweza kutoa ushirikiano wa kutosha.

Thursday, August 1, 2013

Chumba chakutwa na Kondomu "tano"


Chumba cha hoteli ambacho Rose Ndauka alinaswa akiingia na dogo Nasry ambaye ni msanii wa bongo fleva, kimekutwa na kondomu tano zilizotumia...

Rose Ndauka ambaye ni mchumba wa Malik Bandawe, wiki iliyopita alinaswa akiingizwa katika chuba hicho na msanii Nassoro Ayoub "Nasry".


Kwa msaada wa wafanya usafi wa hoteli hiyo iliyoko maeneo ya kinondoni jijini Dar, wawili hao waliingia katika chumba namba G17 cha hoteli hiyo na kutumia masaa takribani matatu huku chumba kikiwa kimefungwa na walipotoka chumba kilikuwa hoi bin taaban....



"Mimi ndiye niliyefanya usafi chumba namba G17 siku hiyo na nilikuta kondomu tano zilizotumika huku shuka zikiwa zimevurugika kabisa."..Alifunguka mfanya usafi huyo

Tukio la binti huyu kunaswa akiingizwa hotelini na dogo Nasry linatia shaka uchumba wake na Malik Bandawe ambaye kwa kipindi kirefu wamekuwa wakitangaza mipango yao ya kufunga ndoa.

Madeni yamuumbua Msanii wa Bongo Movie


STAA wa filamu za Kibongo, Coletha Raymond ‘Koleta’ kwa mara nyingine tena amekumbwa na tuhuma za kukwepa kulipa deni la shilingi 400,000 analodaiwa na staa mwenzake, Husna Iddi ‘Sajenti’..

Kwa mujibu wa chanzo chetu, Koleta alikopa nguo kwenye duka la Sajenti kwa maelezo kwamba angelipa jioni ya siku hiyo lakini mpaka sasa ni miezi saba imepita bila msanii huyo kulipa deni hilo.

Ikazidi kudaiwa kuwa hata Sajenti anapompigia simu Koleta ili kumuulizia kuhusu deni hilo, msanii huyo hapokei simu, hali inayotoa tafsiri kwamba anataka kumdhulumu.

Mwandishi wetu alimtafuta Sajenti ili kupata uhakika kama kweli anamdai Koleta ambapo alifunguka kama ifuatavyo:

“Sijawahi kumuona mtu msumbufu kama Koleta na sasa naanza kuamini maneno ya watu kwamba ana asili ya utapeli,” alisema Sajenti.

Akaongeza kuwa anamdai Koleta tangu mwaka jana na imefikia hatua sasa hapokei simu yake.

“Kinachoniuma ni pale anaposhindwa kupokea simu yangu, nikitumia simu asiyoijua anapokea na akijua ni mimi ananipa ahadi za uongo,” alisema Sajenti.

Mwandishi wetu alimsaka Koleta na kumsomea tuhuma zake ambapo alikubali kudaiwa na Sajenti ila akakanusha kutopokea simu zake, akadai kwamba ameshaongea na msanii huyo ili alipe deni hilo kwa awamu.