Saturday, July 12, 2014

Mke wa mtu ni SUMU....


STAA wa kitambo kwenye tasnia ya filamu za Kibongo, Stanley Msungu amenaswa laivu akiwa kwenye pozi tata na mke wa mtu aliyetambulika kwa jina moja la Bonita.

Tukio hilo lilijiri nje ya Mgahawa wa Great Wall uliopo Masaki jijini Dar, usiku wa saa saba ambapo kulikuwa na tafrija ya chakula cha usiku iliyoandaliwa na Mwenyekiti wa Bongo Movie Unity, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’.

“Dah! Kuna watu wana uhuru kweli na ndoa zao, yaani Bonita amefunga ndoa juzijuzi tu, mumewe amelala nyumbani yeye anahangaika huku na Msungu.

“Kama huamini nenda kwenye gari ukajionee wanachofanya Msungu na Bonita au hadi tufanye sisi ndiyo mnatupiga picha?” alihoji mmoja wa waigizaji walioalikwa kwenye hafla hiyo ambaye jina tunalihifadhi akimsisitiza mwanahabari wetu kwenda kunasa tukio hilo.

Baada ya kunyetishiwa ishu hiyo, Risasi Jumamosi kama kawaida yake lilinyata hadi lilipokuwa gari la Msungu kisha kunasa tukio hilo ambapo Bonita alikuwa akijificha asionekane vizuri huku Msungu akiwa katika hali ya kutaharuki.

“Kaka mke wa mtu huyu, utaniharibia mimi na yeye kwa mumewe, achana na hayo mambo kaka njoo tuzungumze,” alisema Msungu



Friday, July 11, 2014

Dola milioni 35 kugombaniwa fainali kati ya Argentina na Ujerumani


Bingwa mara tatu Ujerumani na bingwa mara mbili Argentina zitagombania dola milioni 35 kwenye mechi ya fainali ya kombe la dunia Jumapili Julai tarehe 13 mjini Rio De Janeiro.

Shirikisho la kimataifa Fifa limetoa jumla ya dola milioni 576 kushindaniwa kwenye mashindano ya mwaka huu nchini Brazil.

Mshindi atajinyakulia dola milioni 35 na wa pili $25 milioni, wa tatu $22 milioni wa nne $20 milioni.

Timu nne zilizoondolewa kwenye robo-fainali zitapokea $14 milioni kila mmoja, timu nane zilizong'olewa raundi ya pili $9 milioni na timu 16 zilizoondolewa raundi ya kwanza $8 milioni kila mmoja.

Ujerumani imefuzu kwa fainali baada ya kuiadhibu Brazil mabao 7-1 na Argentina ikaiondoa Uholanzi mabao 4-2 ya penalti mechi ya nusu-fainali. Kwa jumla timu 32 zimeshiriki mashindano ya mwaka huu kwenye mechi 64 na wachezaji 736 wakajitosa uwanjani.

Miongoni mwa wachezaji nyota kwa upande wa Ujerumani ni mfungaji bora zaidi kwenye mashindano haya Miroslav Klose huku Argentina ikijivunia Lionel Messi mshindi wa tuzo ya mchezaji bora duniani mara nne.

Hii ni mara ya tatu Ujerumani na Argentina wanakutana fainali ya kombe la dunia, mara ya kwanza ikiwa mwaka wa 1986 nchini Mexico Argentina ikashinda 3-2 kisha wakakutana tena mwaka wa 1990 nchini Italia na Ujerumani ikalipiza kisasi kwa kuinyoa Argentina bao 1-0.

Wadadisi wengi wa kandanda wanasema Ujerumani wana nafasi nzuri zaidi ya kuibuka mshindi kwani wameonyesha kiwango cha juu zaidi ya Argentina kufikia sasa.

Lakini mpira unadunda hivyo basi Argentina nao pia waeza kuibuka mshindi ikikumbukwa kwamba hamna timu ya bara Ulaya imewahi kunyakua ubingwa wa dunia mashindano haya yakifanyika Marekani Kusini.

Kwa jumla mataifa ya Marekani Kusini yameibuka mshindi mara tisa kwenye kombe la dunia na ya Ulaya mara kumi Italia na Ujerumani wakiongoza kwa kushinda mara tatu kila mmoja na Brazil ikiwa juu Marekani Kusini kwa kushinda mara tano, Argentina na Uruguay mara mbili kila mmoja.


Wednesday, July 9, 2014

Uholanzi yatupwa nje....


Timu ya Argentina imefuzu kwenda fainali baada ya kuifunga timu ya Uholazi na  kuondoa matumaini yao ya kuweza kunyakuwa ubingwa huo. Timu hizo zilitoka suluhu katika dakika zote na ndipo muda wa penati ulipowadia na timu ya Argentina kupata penati 4 dhidi ya 2 walizopata Uholanzi.

Fainali itakuwa ni kati ya Ujerumani dhidi ya Argentina baada ya hapo jana Ujerumani kuipiga Brazil kipigo cha mbwa mwitu kwa magoli 7 - 1 nakuondoa matumani ya Brazil kulibakisha kombe hilo nyumbani.


Thursday, July 3, 2014

Sakata la Mbasha...


Mambo juu ya mambo! mvumo mkali wenye kuogofya unaendelea kutamalaki katika ndoa ya wanamuziki zao la upako wa Injili Bongo, Emmanuel na Flora Mbasha, safari hii ‘topiki’ siyo zile tuhuma za ubakaji zilizopo mahakamani.



Mbeba ‘niuzi’ wa awamu hii ni Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima, baada ya Mbasha kuona isiwe tabu, hivyo kuamua kupambana na mtumishi huyo wa Mungu kwa njia ya kiroho zaidi.

Mbasha baada ya kulieleza gazeti mama la hili, Uwazi lililoandika habari yenye kichwa “Mbasha: Gwajima Niachie Mke Wangu”, akiidadavua dhana yake kwamba hapendi ufadhili wa Gwajima kwa mkewe, yaani Flora sasa ameamua kwenda mbele zaidi.

Habari zinadai kuwa, mbele ya Mwenyekiti wa Baraza la Maaskofu wa Kipentekoste Mkoa wa Dar es Salaam, Bruno Mwakibolwa ambalo Gwajima ni memba hai, ameshapokea mashitaka kuhusu mchungaji huyo kuhusika kuitikisa ndoa ya waimbaji hao wa Neno la Mungu na mlalamikaji ni Mbasha mwenyewe.
Wikiendi iliyopita, Mbasha aliketi na kiongozi huyo na kushusha tuhuma zake dhidi ya Gwajima kama zilivyothibitishwa na mlalamikaji mwenyewe, nazo ni hizi zifuatazo.

MOSI; Gwajima ni kiongozi wa kiimani wa Mbasha na Flora lakini tangu matatizo ya ndoa yao yalipojitokeza, mchunga kondoo huyo wa Bwana hajawahi kufanya lolote kunusuru muunganiko huo uliohalalishwa kwa jina la aliye juu.



PILI; Gwajima anajua kila kitu kuhusu mgogoro wa Mbasha na mkewe lakini kipindi chote cha matatizo, Kanisa la Ufufuo na Uzima limekuwa mfadhili wa Flora kwa sehemu kubwa. Hapa anauliza, huu ufadhili una kipi nyuma yake?

TATU; Gwajima anatambua kuwa Flora ni mke wa mtu, mwenye mali ameshaomba aachiwe mwandani wake bila mafanikio. King’ang’anizi kina msukumo upi?

NNE; Gwajima amekuwa akimuumiza Mbasha kihisia, kiakili na kiroho kwa sababu yeye anagombana na mkewe lakini mchungaji huyo bila kufikiria maumivu aliyonayo, humwita Flora madhabahuni katika ibada na kumpa nafasi ya kuimba.

TANO; Flora anaishi hotelini na yeye mwenyewe alishakiri kuwa fedha za kulipia hoteli alizipata kutokana na michango ya waumini wa Kanisa la Ufufuo na Uzima. Hapa Mbasha analalamika, inakuwaje kanisa limfadhili mke wa mtu kuishi hotelini ikiwa mumewe hajui?

SITA; Katika hoja zote hizo, Mbasha amelieleza Baraza la Maaskofu wa Kipentekoste kuwa hana imani na Gwajima kwa vile kama ni busara baada ya kuona ndoa hiyo imetikisika yeye (Gwajima) angekaa pembeni kwa namna yoyote ile, hivyo Mbasha akaiomba menejimenti ya baraza hilo kumpa adhabu kali mwenzao.
Mbasha alipozungumza na Amani, Jumanne iliyopita, alisema baraza hilo liliahidi kushughulikia shauri lake na uamuzi utachukuliwa baada ya kumwita Gwajima na kumsikiliza kwa upande wake.

WENYE KWENU KWAHERI!
Kesi ya Mbasha kudaiwa kumbaka shemeji yake ilipoanza, mume huyo wa Flora alikimbilia mafichoni, kwa hiyo swali kwamba anaabudu kwenye kanisa gani halikuwa na mashiko kwa sababu mhusika mwenyewe hakuwa akionekana.

Baada ya Mbasha kujitokeza na kufikishwa mahakamani, kupelekwa mahabusu kwenye Gereza la Keko kabla ya kuachiwa kwa dhamana, ndipo swali kuwa anaabudu kanisa gani lilipoanza kutokana na ukweli kuwa yupo uraiani kwa ‘bondi’.


Swali hilo lilitokana na hoja kwamba kabla ya mgogoro na mkewe walikuwa wakisali kwenye Kanisa la Ufufuo na Uzima linaloongozwa na Gwajima ambaye alishamtuhumu kumfadhili Flora na akamtaka amwachie ‘waubani’ wake huyo ili maisha yaendelee.

Mchungaji

Jawabu la swali hilo, lilijibiwa Jumapili iliyopita baada ya Mbasha kutinga Kanisa la Evangelistic Assemblies of God Tanzania (EAGT), maarufu kama Mito ya Baraka, linaloongozwa na Mchungaji Bruno Mwakibolwa, na kukamilisha haja zake za kuabudu pale.

Mbasha alipozungumza na Amani kuhusu kusali kwa Mchungaji Mwakibolwa badala ya kwa Gwajima, alijibu: “Nimehama Kanisa la Ufufuo na Uzima, sisali tena kule. Kuanzia sasa shughuli zangu za kuabudu nitazifanyia Mito ya Baraka kwa Mchungaji Mwakibolwa.

“Siwezi kwenda kwa Gwajima kwa sababu simuelewi na ndiyo maana nimeamua kumshtaki kwa Baraza la Maaskofu wa Kipentekoste. Roho yangu ya kuabudu isingekuwa timilifu, ingejaa mashaka kwenda sehemu ambayo imenijeruhi na nisiyoiamini.

“Kwa kifupi si kwamba nimeanza kuabudu Mito ya Baraka hili ndilo kanisa letu tangu zamani, mimi na mke wangu. Tulihamia Kanisa la Ufufuo na Uzima baada ya Gwajima kutushawishi, kwa hiyo nimerejea kundini.
MCHUNGAJI MWAKIBOLWA
Juzi, Amani lilimsaka Mwenyekiti wa Baraza la Maaskofu Mkoa wa Dar es Salaam, Mchungaji Mwakibolwa lakini simu yake ilipokelewa na kusikika sauti za watu wakiwa kwenye maombi kama si ibada.
GWAJIMA
Baada ya hapo, Amani lilimsaka Mchungaji Gwajima kwa njia ya simu yake ya mkononi lakini yeye hakupokea hata pale alipopigiwa kwa kurudiarudia.
KESI YA MBASHA
Kesi ya Mbasha kudaiwa kubaka itatajwa tena Julai 17, mwaka huu kwenye Mahakama ya Wilaya ya Ilala, Dar es Salaam.
VIPI KUHUSU KUPATANA?
Wiki iliyopita katika Gazeti la Risasi Jumamosi kuliandikwa habari yenye kichwa; MBASHA, FLORA WAPATANA. Katika habari hiyo ilidaiwa wawili hao walipatana lakini walibakiza kikao kimoja cha kumalizia taratibu zote.

Habari zinasema, taratibu hizo zinandelea licha ya Mbasha kumshitaki Gwajima kwenye Baraza la Maaskofu wa Kipentekoste Mkoa wa Dar es Salaam.

Source: Global Publisher

Flora hofu tupu....


Hivi karibuni mumewe, Hamis Baba ‘H. Baba’ kuugua ugonjwa wa homa ya Dengue ‘Dengi’ na kulazwa Muhimbili, msanii wa filamu Bongo, Flora Mvungi amesema alijikuta kwenye wakati mgumu kuhofia mumewe angepoteza maisha.


Flora alisema ni Mungu tu mumewe kupona kwani alikuwa katika hali mbaya ambayo mpaka yeye kama mkewe alikuwa na hofu kubwa ya kifo haswa ukizingatia vifo vya wasanii vilivyotokea mfululizo.

“Nilipoona wasanii wenzangu wakifariki dunia na mume wangu kuzidiwa mpaka kulazwa Muhimbili, nilikuwa nina hofu kubwa ya kifo lakini namshukuru Mungu amepona na tunaendelea na maisha kama kawaida, dengue noma sana,” alisema Flora.

Wednesday, July 2, 2014

Wakazi wa Manyoni waiomba serikali kuwatatulia tatizo la maji.


Wakazi wa vijiji vya MAKALE, MITUNDU, MGANDU na ITIGI wilayani MANYONI mkoa wa SINGIDA wameiomba serikali kufanya juhudi za ziada kuwatatulia tatizo la maji katika maeneo yao.

Wakazi hao wamesema tatizo la maji limedumu kwa zaidi ya miaka 30 hali ambayo huwalazimu kukesha usiku kucha wakitafuta maji.

Wakazi hao wametoa kilio hicho mbele ya Naibu Waziri wa Maji AMOS MAKALA aliyetembelea vijiji mbali mbali wilayani Manyoni ili kukagua hali ya upatikanaji wa huduma ya maji.

Akijibu malamiko ya wananchi hao MAKALA amesema serikali inashughulikia tatizo la maji na hadi mwaka huu utakapokamilika tatizo hilo litakuwa limepatiwa ufumbuzi.


NGORONGORO: Migogoro ya wafugaji kutatuliwa.



Waziri wa Maliasili na Utalii, LAZARO NYALANDU ameagiza bodi ya Mamlaka ya NGORONGORO kutatua migogoro ya wafugaji wanaoishi katika bonde la hifadhi ya NGORONGORO kufuatia wafugaji hao kufunga bara bara kwa madai ya kupinga kujengwa kwa hoteli ya kitalii katika hifadhi hiyo bila kushirikishwa.

Akizungumza na wafugaji hao Waziri NYALANDU amesema serikali haitaruhusu ujenzi wowote ufanyike katika eneo hilo kwa sasa mpaka hapo tathmini itakapofanywa na ofisi ya makamu wa Rais mazingira na kubaini iwapo ujenzi huo ufanyike au la.

Waziri Nyalandu ambaye alikwenda NGORONGORO kuzindua bodi mpya ya hifadhi ya NGORONGORO amesema ni vema bodi hiyo ikatafuta mbinu za kutatua migogoro katika sehemu ya hifadhi.

Kuhusu suala la uwakilishi zaidi wa wafugaji katika bodi ya NGORONGORO amesema ndani ya siku SABA atateuwa mwakilishi mwingine toka katika jamii hiyo ili aweze kuingia katika bodi hiyo na hivyo kufanya idadi ya wawakilishi WAWILI.