Wednesday, July 2, 2014

Watu 18 wauawa katika mlipuko Nigeria.




Takriban watu 18 wameripotiwa kuuawa katika mlipuko uliotokea sokoni mjini Maiduguri Kaskazini mwa Nigeria.
Watu walioshuhudia tukio hilo wamesema kuwa gari lililokuwa limebeba mkaa lilipuliwa na bomu linalodhaniwa liliwekwa ndani ya gari hilo.
Hadi sasa hakuna kundi lolote la kigaidi lililokiri kufanya shambulio hilo.

Tukio hili linakuja huku ripoti ya hivi karibuni ya jeshi la Nigeria ikisema kuwa limeshambulia moja ya ngome za kundi la wapiganaji la Boko Haram.

Serikari kutaifisha mashamba yasiyoendelezwa Tanga.


Waziri mkuu mheshimiwa Mizengo Pinda ameuagiza uongozi wa serikali mkoa wa Tanga kuorodhesha mashamba yote yasiyoendelezwa kisha kuwasilisha kwake ili aweze kumkabidhi mheshimiwa Rais aweze kutoa maamuzi kufuatia baadhi ya wawekezaji kuhodhi maeneo makubwa na kusababisha wananchi kukosa mashamba ya kulima.
Mheshimiwa Pinda ametoa agizo hilo wakati akihutubia mamia ya wakazi wa mkoa wa Tanga katika kilele cha maonesho ya biashara ya halmashauri zote nchini yaliyofanyika kitaifa jijini Tanga kisha washindi kukabidhiwa tuzo kama ishara ya kuvutia wawekezaji.
 
Kuhusu mchakato wa uchaguzi mkuu ujao waziri Pinda amewaagiza viongozi wa kuanzia serikali za mitaa na vijiji,kata,tarafa hadi wilaya na taifa kwa ujumla kuwaelimisha wananchi kuhusu umuhimu wa kuchagua viongozi wenye sifa katika uchaguzi mkuu ujao wa serikali za mitaa ili kulinda Demokrasia ya kweli kwa watanzania.
 
Awali mwenyekiti wa jumuiya ya tawala za serikali za mitaa nchini (ALAT) Dr,Didas Masaburi amesema jumuiya haitamuunga mkono mgombea kuanzia ngazi ya Rais,Ubunge na Diwani endapo atashindwa kusimamia mchakato wa ugatuaji madaraka kwenda kwa wananchi ili kuleta demokrasia ya kweli.
 
Katika hitimisho la maonesho ya biashara ya halmashaurio zote nchini waziri mkuu alitoa zawadi kwa washiriki washindi wa maonesho hayo ambayo halmashauri ya jiji la Tanga iliibuka kidedea kwa kushika nafasi ya kwanza ikifuatiwa na halmashauri ya Bukoba.

Tuesday, July 1, 2014

It's half time....


Kipindi cha kwanza kimeisha huku timu zote zikitoka bila kufungana.

Endelea kutuma comments zako kuwa nani atafanikiwa kufuzu katika Robo fainali ya Kombe la Dunia 2014

Endelea kuwa nasi kwa taarifa zaidi.

Hivi punde Belgium Vs USA...


Hivi ndivyo Makocha wa kila timu alivyo panga kikosi chake kukabiliana na mpinzani wake.

Kila timu inahitaji kuendelea mbele ya mashindano haya, Je ni Belgium ama USA watakao endelea mbele ya mashindano haya ( Robo fainali )?

Usikose mtanange huu.....

Mwenge wa uhuru umeendelea na mbio zake katika mkoa wa NJOMBE


Mwenge wa uhuru umeendelea na mbio zake katika mkoa wa NJOMBE kwa kukimbizwa katika wilaya ya WANGING’OMBE ambako kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Mwaka huu RACHEL KASSANDA amewataka watanzania kuwapuuza wanasiasa wanaowapotosha wananchi wasishiriki katika shughuli za Maendeleo.

KASSANDA ametoa wito huo baada ya kuzindua, kufungua na kuweka mawe ya Msingi katika Miradi TISA ya maendeleo ambayo wananchi wa WANGING’OMBE wamechangia nguvu zao katika ujenzi wake.

Amesema watanzania wasikubali kuibomoa nchi yao bali wailinde waipiganie na kuitetea dhidi ya wanaoichafua

Usikose mtange huu.....


Ni baada ya Uswizi kutupwa nje ya mshindano hayo na timu ya Argentina kwa bao moja bila majibu. Mtanange huo ulimalizika katika dakika zote tisini bila kumpata mbabe na ndipo timu ya Argentina kupitia kwa mchezaji wake DI MARIA ilipata goli la kwanza na la ushindi katika dakika thelathini za nyongeza.

Saa tano kutakupa na pambano kati ya Belgium na USA. Je ni nani kati ya timu hizi mbili atafuzu kwenda Robo finali?

Toa comments zako juu ya mtanange huu.

Serikali inaendelea na maandalizi ya uchaguzi wa Serikali za mitaa


Waziri Mkuu MIZENGO PINDA amesema serikali inaendelea na maandalizi ya uchaguzi wa Serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika nchini mwezi Oktoba mwaka huu.

Akizungumza mkoani TANGA na mameya wa majiji, manispaa na wenyeviti wa Halmashauri za Miji na Wilaya nchini, Waziri Mkuu PINDA amesema hata hivyo hatma ya kufanyika kwa uchaguzi huo inategemea kukamilika kwa mchakato wa Katiba mpya.

Waziri Mkuu amesisitiza suala la ukusanyaji mapato na udhibiti wa matumizi ya fedha za serikali na kuongeza kuwa amewaandikia barua Wakuu wa Mikoa akiwataka waweke utaratibu wa kutoa taarifa kila baada ya miezi mitatu juu ya makusanyo ya kila Halmashauri zilizo kwenye mikoa yao.